Ukraine imehifadhi ushahidi kuhusiana na kunyongwa kwa wafungwa 93 wa vita wa Ukraine kwa mujibu wa afisa wa sheria aliyepewa jukumu la kuchunguza uhalifu wa kivita unaohusiana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine.
Yuriy Belousov ambaye anaongoza idara ya Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu anayehusika na uchunguzi wa uhalifu uliofanywa katika vita vya kutumia silaha alitoa takwimu ya hivi karibuni wakati alipozungumza na vyombo vya habari moja kwa moja siku ya Ijumaa.
"Sasa tuna habari kuhusu vifo vya wanajeshi wetu 93 ambao waliuwawa kwenye uwanja wa vita" Belousov aliiambia Yedyniy Novyny, matangazo ambayo yanaunganisha chaneli nyingi za televisheni za Ukraine.