Ukraine, Jumapili imefungua uchunguzi wa makosa ya jinai baada ya shambulio la kombora la Russia, kuwaua wanajeshi kadhaa katika kile vyombo vya habari vinasema ilitokea wakati wa “sherehe ya kukabidhi tuzo” katika uwanja wa mapambano wiki hii.
Takriban wanajeshi 20 wameripotiwa kuuawa katika shambulizi hilo, ambalo vyombo vya habari vya nchi hiyo vilisema kuwa lilifanyika Ijumaa wakati brigedi ilikusanyika kupokea tuzo katika mkoa wa Zaporizhzhia kusini mwa Ukraine.
“Hili ni janga ambalo lingeweza kuepukwa,” Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, alisema katika hotuba yake ya Jumapili jioni.
Uchunguzi wa uhalifu huo umeanzishwa aliongeza kusema.
AFP haikuweza kuthibitisha mara moja mazingira ya shambulizi hilo ama idadi ya watu waliouawa.
Jeshi la Ukraine lilithibitisha Jumamosi kwamba idadi ya wanajeshi kutoka kikosi chake cha 128 cha mashambulizi ya milimani waliuawa katika shambulizi.