Ukraine yafanya maombolezo kwa vifo vya watu 37

Ukraine Jumanne, imetangaza siku ya maombolezo wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipokutana katika mkutano wa dharura, kufuatia msururu wa makombora ya Russia, yaliyoua takriban watu 37 na kujeruhi wengine zaidi ya 170.

Miongoni mwa malengo ya shambulizi la Jumatatu la miji kadhaa, ilikuwa hospitali kubwa zaidi ya watoto nchini humo, sehemu ya mfululizo wa mashambulizi ya mchana ambayo Meya Vitali Klitschko, alielezea kuwa mojawapo ya mashambulizi zaidi katika vita hivyo.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, amelaani vikali shambulizi hilo na kusema kwamba Russia, lazima iwajibike.

Siku ya Jumanne, pembezoni mwa mkutano wa NATO ulioanza hapa jijini Washington, Rais Zelenskyy aliiambia VOA kwamba atazungumza na viongozi.