Ukraine yadai ni Russia iliyoathiri kubadilishana wafungwa

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, Jumanne amesema kupungua kwa hivi karibuni kwa mabadilishano ya wafungwa na Moscow kulitokana na sababu zisizojulikana kwa upande wa Russia, lakini alielezea  matumaini kwamba ubadilishaji huo unaweza kuanza tena hivi karibuni.

Pande hizo mbili zimefanya mabadilishano kadhaa ya wafungwa katika miezi ya mwanzo ya uvamizi wa Russia, nchini Ukraine, Februari 2022 na hadi mwaka huu. Lakini kasi ya mabadilishano ilipungua 2023, na mara ya mwisho ilifanyika mapema Agosti.

Mwezi uliopita kamishna wa haki za kibinadamu wa Ukraine, Dmytro Lubinets, amesema wafungwa wa Russia, nchini Ukraine walikuwa wameonyesha nia ya kubadilishana lakini Moscow haikuwa tayari kuwarejesha.