Ukraine inasema mashambulizi ya Russia yameua watu 7 mjini Kharkiv

  • VOA News

Picha hii inaonyesha jengo kubwa la makazi ya watu likiwaka moto kufuatia shambulio la kombora mjini Kyiv, Februari 7, 2024. Picha ya AFP

Ukraine imesema mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani za Russia kwenye mji mkubwa wa pili wa Ukraine wa Kharkiv, yaliua watu 7 Jumamosi, wakiwemo watoto watatu na kusababisha moto ulioharibu nyumba na majengo mengine ya raia.

Ndege zisizokuwa na rubani Ijumaa zililenga majengo ya raia ndani na karibu na Kharkiv, maafisa wamesema, na kuua watu 7 wakiwemo watoto watatu.

Gavana wa mkoa huo Oleh Synehubov aliandika kwenye mtandao wa Telegram kwamba ndege zisizokuwa na rubani ziliharibu majengo ya raia katika wilaya ya Nemyshlianskyi.

Shambulio hilo la ndege zisizokuwa na rubani zilizotengenezwa na Iran lilisababisha moto mkubwa ambao uliharibu takriban nyumba 14 za watu binafsi.

Jeshi la anga la Ukraine limesema lilitungua ndege zisizo na rubani 23 kati ya 31.