Ukraine imesema leo Alhamisi kuwa kitengo chake cha ulinzi wa anga kilitungua ndege zote 42 zisizokuwa na rubani ambazo Russia ilizitumia katika mashambulizi ya usiku kucha ikilenga mikoa mbalimbali nchini humo. Jeshi la anga la Ukraine limesema pia lilitungua kombora lililoongozwa na Russia.
Mashambulizi ya ya drone za Russia yalielekezwa katika mikoa ya Cherkasy, Dnipropetrovsk, Kherson, Kirovohrad, Kyiv, Mykolaiv, Rivne, Vinnytsia, na Zhytomyr. Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema imeharibu ndege mbili zisizo na rubani za Ukraine katika mkoa wa Kursk, na Drone nyingine katika mkoa wa Belgorod.
Mapambano ya anga yamekuja siku moja baada ya ndege isiyo na rubani ya Ukraine kupiga ghala katika mkoa wa Tver nchini Russia, na kusababisha moto mkubwa na kuwalazimisha watu kuhamishwa katika eneo hilo.