Ukraine imeanza mashambulizi ya kukomboa sehemu zilizochukuliwa na Russia

Waziri wa ulinzi w Ukrine Oleksii Reznikov ( April 21, 2023

Ukraine imeonekana kuanza mashambulizi ya kujaribu kudhibithi tena sehemu za mashariki na kusini mwa nchi hiyo ambazo zilidhibitiwa na Russia katika wiki za kwanza za vita, zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Serikali ya Kyiv haijasema lolote kuhusu shughuli za jeshi lake katika sehemu za vita lakini mashambulizi makali yameanza kusini mwa nchi hiyo katika maeneo ya Zaporizhzhia.

Russia imesema kwamba imezuia jaribio la kwanza la wanajeshi wa Ukraine kuingia sehemu hiyo.

Maafisa wa Ukraine wamesema leo Ijumaa kwamba jeshi lake limeangush mkombora manne ya Russi na ndege 10 zisizokuwa na rubani, katikati mwa Ukraine.

Ofisi ya rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa, imesema kwamba Ramaphosa amezungumza na rais wa Russia Vladimir Putin kuhusu ziara inyotarajiwa ya viongozi wa Afrika wanaotaafuta kumaliza vita vya Ukraine kwa njia ya diplomasia.