Ukame wa mvua unaleta tishio la njaa Zimbabwe

Mmoja wa wakulima Zimbabwe

Idara ya Umoja wa Mataifa ya mpango wa chakula duniani ilisema inahitaji dola milioni 75 kuhakikisha kuwa usalama wa chakula nchini humo lakini hadi sasa wamepokea theluthi moja tu ya kiwango hicho

Ukame wa muda mrefu katika eneo la kusini magharibi mwa Zimbabwe umesababisha ukosefu wa usalama wa chakula na mifugo ambayo ni chanzo kikuu cha maisha inajitahidi kuishi huku wakazi wakitembea mwendo mrefu sana kutafuta maji. Idara ya Umoja wa Mataifa ya mpango wa chakula duniani ilisema inahitaji dola milioni 75 kuhakikisha kuwa usalama wa chakula nchini humo lakini hadi sasa wamepokea theluthi moja tu ya kiwango hicho.

Uhaba wa mvua watishia ukame Zimbabwe

Matopo iko kiasi cha kilometa 600 kusini magharibi mwa mji mkuu Harare katika mkoa wa Matebeleland ambako mazao kwa kawaida hushindwa kumea kwasababu ya mvua kidogo. Hivyo wanyama katika mkoa huu wenye hali ya ukavu siyo tu dalili ya utajiri lakini chanzo cha maisha; wanauzwa au kubadilishwa kwa nafaka hasa mahindi ambayo hutumika kutayarisha chakula kikuu nchini humo maarufu kama SADZA au uji ISITSHWALA.

Wafugaji wanakwenda kutafuta maji kwa ajili ya mifugo yao kama vile kwenye bwawa la Mabigwe ambalo nalo limekauka.

Wafadhili wanasema kuwa watafika kufanya matengenezo kwenye bwawa, lakini hawajafika. Hakuna hata mmoja anayefika kufanya matengenezo. Kwahiyo maji yanapomalizika hapa lazima tutembee mwendo mrefu kwa ajili ya kuwapatia ng’ombe wetu maji ya kunywa.

Baadhi ya wanavijiji huko Zimbabwe

Wengine wanachimba kupata maji kwa ajili ya ng’ombe wao, lakini msimu wa kiangazi unapoendelea, visima ambavyo havina kina kirefu navyo vinakauka, mambo si mazuri hata kidogo alisema Mpumelo Dungeni. “Ukame mwaka huu umekuwa mbaya sana. Ng’ombe wetu wanakufa kwasababu hawana maji ya kutosha ya kunywa. Tunatembea mwendo mrefu ili kuhakikisha ngo’ombe wanapata maji waishi. Tunaiomba serikali kuingilia kati na kutatua tatizo letu la maji. lazima walitengeneze hili bwawa. Hatujaiona serikali. Tunawaona nyinyi na tuna matumaini mtawapelekea huu ujumbe”.

Maafisa wa serikali ya Rais Emmerson Mnangagwa mjini Bulawayo mji ulio karibu na sisi ambako taasisi za misaada kwa kawaida huwa zinakwenda kuwasaidia wanavijiji.

Shirika la mpango wa chakula duniani linasema linahitaji dola milioni 75 kuhakikisha usalama wa chakula wakati wa msimu ambao mavuno ni machache nchini Zimbabwe kwa kipindi cha miezi sita ijayo. USAID program ya chakula kwa amani imetoa dola milioni 22. Ilieleza hivi sasa ukosefu wa usalama wa chakula unachangiwa na vipindi virefu vya kiangazi katika msimu wa mvua wa mwaka 2017 hadi 2018 katika baadhi ya maeneo ya Zimbabwe.

WFP

Mkurugenzi wa WFP Zimbabwe, Eddie Rowe alisema Zimbabwe inakadiriwa hivi sasa ina asilimia 28 ya idadi ya watu wanaoishi vijijini ambao wanakumbwa na changamoto kubwa linalokuja suala la kupata fursa ya chakula katika msimu huu wa kilimo wa mwaka 2018 – 2019. Tunazungumzia watu milioni 2.4 ambao hawana chakula kwasababu hawana uwezo au wanashindwa kukidhi mahitaji ya majumbani mwao.

Wakati wa msimu wa mvua chache ambao utaendelea hadi mwezi May 2019, WFP inasema inafanya kazi kuzungumzia mahitaji ya haraka sana ya chakula.