Ripoti ya umoja wa mataifa inasema kwamba waathirika wana umri kati ya miaka nane na 75.
Kiwango kikubwa cha ukatili kimetekelezwa na kikosi cha RSF kinachoungwa mkono na wapiganaji wa kiarabu katika jaribio la kuwaadhibu raia kwa kushirikiana na wale wanaowachukulia kuwa maadui.
Kikosi cha RSF kinapigana na jeshi la Sudan. RSF hawajajibu shutuma za ripoti ya umoja wa mataifa.
Wapiganaji wa RSF wanadhibithi sehemu kubwa ya Sudan ikiwemo Dafur Magharibi, amabako wanashutumiwa kwa mauaji ya kijamii dhidi ya watu wa Masalit.