Ujerumani yataka kuimarisha uhusiano wake na Mali

Rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita, mwenye kanzu akiwa naChansela wa Ujerumani Angela Merkel (R)

Chansela wa Ujerumani, Angela Merkel alisema Jumapili kwamba Ujerumani inataka kuimarisha uhusiano wake na nchi ya Mali ili kuboresha maendeleo katika taifa hilo la Afrika magharibi lisilo thabiti na kulisaidia kupambana dhidi ya wenye msimamo mkali na kuhakikisha linatekeleza mkataba wa amani.

Rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita alimpokea bibi. Merkel kwenye uwanja wa ndege wa Bamako mahala ambako alizungumza matamshi hayo kabla ya kuwa na mkutano na rais huyo pamoja na maafisa wengine na wawakilishi wa Ujerumani kwenye operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa nchini Mali.

Bibi. Merkel anatarajiwa kulenga juu ya utekelezaji wa mkataba wa amani ulioafikiwa mwezi June mwaka 2015 kati ya serikali ya Mali, kundi la wanaojitenga la watuareg pamoja na makundi mengine yenye silaha huko eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.