Ujerumani kuanza mgao wa mafuta

Vituo vya mafuta nchini Ujerumani

Ujerumani imetangaza rasmi kuanza kutoa gesi kwa watu wake kwa mgao, huku kukiwepo wasiwasi ya kuacha kuagiza mafuta kutoka Russia.

Hatua hiyo imechukuliwa wakati kuna hali ya kutoelewana kuhusu malipo kwa kutumia sarafu ya Russia.

Hatua ya umoja wa ulaya kuanza kutekeleza onyo la mapema la uwezekano wa kutokea uhaba wa gesi, ni ishara ya moja kwa moja ya kutokea uhaba wa mafuta kutokana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine.

Waziri wa uchumi wa Ujerumani Robert Habeck, ameambia waandishi wa habari kwamba chumba cha dharura kitaundwa ndani ya wizara hiyo, akiongezea kwamba timu itakayosimamia swala hilo itahusisha wanachama kutoka kwa wizara hiyo, wasimamizi wa mafuta nchini humo na wadau kutoka sekta binafsi.

Katika hatua inayoonekana kama juhudi za kuimarisha sarafu yake ambayo inaendelea kupoteza thamani, Russia imesema kwamba itaweka mikakati ifikapo March 31, ambapo nchi ambazo zimetajwa kwamba sio rafiki, zile ambazo zimeiwekea vikwazo, zitalipia gesi yake kwa kutumia sarafu ya Russia na wala sio Euri wala dola ya Marekani.

Moscow inatarajiwa kuzindua kanuni mpya kuhusu malipo ya gesi kesho alhamisi.

Kremlin imesisitiza kuhusu mfumo kwa malipo ya gesi kwa umoja wa ulaya, baada ya mawaziri kutoka nchi 7 tajiri duniani kutaja mpangilio huo kuwa usiokubalika.

Uvamizi wa Ukraine imepelekea Russia kuwekewa vikwazo kadhaa na kupelekea sarafu yake kushuka kwa thamani huku Ulaya ikisitisha uagizaji wa mafuta na gesi kutoka Russia.