Uingereza yasema haitafanya mashauriano kuhusu malipo na chama cha wauguzi

Waziri wa afya wa Uingereza, Steve Barclay, Jumapili amesema serikali haitafanya mashauriano  kuhusu malipo na chama cha wauguzi, huku tishio la migomo likiongezeka.

Ombi la serikali, ambayo ni pamoja na malipo ya mara moja sawa na asilimia 2 ya mishahara katika mwaka wa fedha wa 2022 - 2023 na nyongeza ya asilimia 5 kwa mwaka 2023 - 2024, lilikataliwa na wanachama wa chuo cha uuguzi cha Royal mwezi Aprili.

Alipoulizwa na shirika la habari la Sky News kama serikali ingeanzisha tena mazungumzo na chama cha wafanyakazi, Barclay alisema, “sio kuhusiana kiwango cha malipo.”

Muungano huo tayari unawategemea wanachama wake 300,000 kuchukua hatua zaidi za mgomo katika kipindi cha miezi sita ijayo. Muungano huo haukujibu maombi ya shirika la habari la Reuters kutoa maoni yake kwa matamshi ya Barclay ya Jumapili.