Hatua hiyo inadhihirisha mwanza wa utekezaji wa sera ya uhamiaji ya waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak.
Sheria kufanikisha hatua ya kuwatuma wahamiaji nchini Rwanda wanapowasili Uingereza bila idhini, ilipitishwa bungeni mwezi April, na Sunak anataka ndege ya kwanza yenye wahamiaji hao kuanza safari mwezi Julai.
Zaidi ya wahamiaji 7,500 wamewasili Uingereza wakitumia boti ndogo kutoka Ufaransa mwaka huu.
Serikali imesema hatua hiyo itawazuia wahamiaji kufasiri kwa njia hatarishi baharini kuelekea Uingereza.
Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yamepinga sera hiyo na kesi kadhaa zinatarajiwa mahakamani kuipinga.
Shirika la kuwashughulikia wakimbizi la Care4Calais, limesema ukamataji ulianza Jumatatu wiki hii.