Russia ikionekana kuhamishia mashambulizi yake ya kijeshi kutoka mji mkuu wa Ukraine wa Kyiv na kuelekea mashariki mwa nchi hiyo.
"Uhuru wako ni wetu," Biden alimwambia mwenzake wa Poland.
Poland, mwanachama wa NATO, imepokea zaidi ya wakimbizi milioni mbili wa Ukraine. Biden, akifuatana na Meya wa Warsaw Rafal Trzas-kowski, amekutana na baadhi ya wakimbizi hii leo Jumamosi ili kujadili juhudi za misaada ya kibinadamu.
Duda, ambaye nchi yake inapakana na Ukraine, alisema "uhusiano wa Poland na Marekani unastawi" na vita vya Russia dhidi ya Ukraine vinasisitiza umuhimu wa NATO iliyoungana.
"Poland wana hisia kubwa ya hatari kwa sababu tunajua nini maana ya ubeberu wa Russia na shambulio la jeshi la Russia. Kwa sababu babu na babu zetu, wakati mwingine wazazi wetu, walinusurika," Duda alisema.
Poland, mwanachama wa NATO, imekubali zaidi ya milioni 2 kati ya wakimbizi milioni 3.8 wa Ukraine ambao wameikimbia nchi yao, na hivyo kuzua mzozo wa kibinadamu ambao Biden pia alijadiliana na maafisa wa Poland.