Uhasama kati ya India na China umeongezeka, maelfu ya wanajeshi wakiwa wameshika doria kwenye mpaka wenye mzozo wa Himalaya, kwa muda wa miaka mitano sasa.
Hata hivyo, biashara kati ya nchi hizo mbili imeongezeka.
Wataalam wanasema kwamba India ina wasiwasi kuhusiana na miradi ya ujenzi wa reli na barabara pamoja na mifumo ya kijeshi inayotekelezwa na China katika Himalaya.
Uhusiano kati ya India na China uliharibika sana baada ya mapambano ya kijeshi ya mwezi Juni 2020.
Tangu wakati huo, karibu wanajeshi 50,000 wenye silaha nzito na ndege za kivita, kutoka pande zote wanashika doria kwenye mpaka wa Himalaya usiokuwa na alama za kutambuliwa kwa urahisi kutofautisha kila upande.