Uganda kuchangamkia fursa mpya za kibiashara DRC

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Felix Tshisekedi (kushoto) akiwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika ziara yake nchini Uganda, November 9, 2019. (Photo by

Baada ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuingizwa rasmi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, wafanyabiashara na wajasiriamali nchini Uganda wamehamasika na fursa zitakazoletwa na kujiunga huko.

Congo inaongeza zaidi ya watu milioni 90 katika Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye watu milioni 177. Katika ukanda huo, Uganda ni nchi ya pili kwa usafirishaji mkubwa zaidi wa bidhaa kwenda Congo, baada ya Rwanda.

Wananchi wa Afrika Mashariki hivi sasa wanaweza kuwa huru kusafiri kwenda Congo iwapo vikwazo vya kusafiri na biashara kama vile dola 50 ya visa vimeondolewa. DRC inashirikiana mipaka na nchi zote za Afrika Mashariki isipokuwa Kenya.

Reagan Mugume wa Kituo cha Utafiti wa Sera za Uchumi, aliyeko Kitengo cha Biashara Chuo Kikuu cha Makerere, alisema Uganda na Rwanda wana nafasi nzuri ya kutumia kwa maslahi yao fursa zilizoko DRC kwa sababu ya ukaribu wao kijografia na mahusiano ya huko nyuma ya kibiashara na nchi hiyo.

Ukuaji wa Biashara

Mnamo mwezi Januari, biashara kati ya Uganda na DRC ilifikia kiwango cha juu, wakati fursa mpya za masoko zilipofunguka kwa bidhaa za Kampala.

Kulingana na takwimu za Januari 2022 kutoka Benki Kuu ya Uganda, Kampala inasafirisha kwenda DRC bidhaa za thamani ya dola milioni 74.3 kwa mwezi huo, juu zaidi kutoka dola milioni 29.9 mwezi Disemba 2021, ikiwasilisha ukuaji wa asilimia 44.

Takwimu za Januari ziko juu kuliko pato la mauzo ya nje kutoka Kenya, ambayo imekuwa kihistoria ni mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara na Uganda. Uganda ilikusanya dola milioni 40.9 kutokana na kuiuzia Kenya bidhaa zake katika mwezi huo huo.

Vitu vikuu ambavyo Uganda inaiuzia DRC ni pamoja na Simenti, mafuta ya mawese, mchele, sukari, petroli iliyosafishwa, bidhaa zilizopikwa, vipodozi na vifaa vya chuma.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la The East African, Kenya