Uganda yapeleka jeshi Karamoja kudhibiti wafugaji wenye silaha

Kijana wa kiume akichunga mbuzi huko Karamoja, Uganda ambako wakazi wa huko hujishughulisha na ufugaji na kilimo.

Kijana wa kiume akichunga mbuzi huko Karamoja, Uganda ambako wakazi wa huko hujishughulisha na ufugaji na kilimo.

Jeshi limeripoti kuwa wafugaji wawili walioshambulia maafisa wa jeshi la Uganda katika eneo la Kamioni waliayani Kaboong walipatikana na bunduki tatu aina ya AK 47.

Idadi kubwa ya wanajeshi wa Uganda wamepelekwa mpakani mwa Uganda na Kenya, maeneo ya Karamoja, ili kutekeleza azma ya serikali ya kuwaondoa wafugaji wa jamii ya Turkana kwani baadhi yao wanahatarisha usalama wa nchi.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili ya VOA, Kennes Bwire ameripoti kuwa hatua hii imechukuliwa na serikali ya Uganda baada ya kubainika kuwa wa Turkana kutoka Kenya, wanafanya biashara ya bunduki katika eneo la Karamoja.

Ameendelea kusema kuwa hatua ya jeshi la Uganda (UPDF) kuwafukuza wafugaji hao inafuatia kitendo cha wafugaji hao kukataa kufuata sheria za nchi ikiwa pamoja na kutoingia Uganda na bunduki.

Mkuu wa wilaya ya Moroto

Akizungumza na VOA mkuu wa wilaya ya Moroto eneo la Karamoja, anayesimamia kamati ya usalama eneo hilo, Peterson Ken, amesema idadi kubwa ya wanajeshi wa Uganda, wanaendelea kushika doria katika maeneo ya Kotido, Abim, Kaboong , Agago, Moroto, Amudat, Nakapiripirit, Napak, Sebei, Busoga na Teso.

Aliongeza kuwa kwenye mpaka wa Uganda na Kenya, tayari wanajeshi hao wamewafukuza wafugaji hao na mifugo yao na kuhakikisha kwamba hakuna wengine watakaoingia Uganda kinyume cha sheria.

Jeshi la Uganda na viongozi katika maeneo ya Karamoja, wanaripoti kwamba wafugaji kutoka Kenya wamekataa kufuata masharti ya nchi na hata kupigana na maafisa wa usalama.

Jeshi limeripoti kuwa wafugaji wawili walio washambulia maafisa wa jeshi la Uganda katika eneo la Kamion wilayani Kaboong walipatikana na bunduki tatu aina ya AK 47.

Wafugaji walisha mifugo yao Uganda

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Uganda, Luteni Paddy Ankunda

Jumla ya wafugaji 50,000 wa jamii ya Turkana kutoka Kenya, waliingia nchini Uganda mwishoni mwa mwaka jana kulisha mifugo ipatayo 90,000 kutokana na hali ya kiangazi kaskazini magharibi mwa Kenya.

Ameeleza waliruhusiwa kulisha mifugo katika maeneo ya Kobebe wilayani Moroto, Loyoro, Kamion na Kalapata wilayani Kaabong.

Serikali ya Uganda ilifanikiwa kuwapokonya bunduki raia wake, wafugaji wa jamii ya Karamojong baada ya kampeni ya miaka kadhaa, kwani wakaramojong walikuwa wakitumia bunduki hizo kutekeleza uhalifu, aliongeza.