Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa-UNHCR lilisema Jumanne kwamba wafadhili wake watazuia msaada wa fedha kwa operesheni za Uganda hadi idadi ya wakimbizi ithibitishwe baada ya shutuma kwamba maafisa waliongeza idadi ya halali ya wakimbizi ili waibe fedha za ziada.
Uchunguzi mbali mbali unafanywa na serikali ya Uganda, Umoja wa Mataifa na umoja wa ulaya kuhusiana na shutuma hizi kwamba msaada umekuwa ukiibwa. Wachunguzi pia wanaangalia iwapo chakula na vifaa vingine vya msaada vilivyolengwa kwa wakimbizi viliuzwa, vilitolewa kwa hongo, pamoja na usafirishaji haramu kwa wakimbizi wasichana.
Tayari wiki iliyopita serikali ya Uganda imeshachunguza uwezekano wa makosa yaliyotokea na kufanywa na maafisa wake, ilisema inapanua mashtaka kuona kama wafanyakazi kutoka Umoja wa Mataifa, UNHCR na program ya chakula duniani-WFP walidaiwa kuhusika na rushwa ya wafanyakazi wa serikali ya Uganda.