Shirika la Global Witness lashutumu Liberia imegubikwa na rushwa kwenye sekta ya mafuta kupelekea makampuni yasio na uzoefu kupewa mikataba.
Shirika la kimataifa la uangalizi linaonya kwamba ufisadi tayari umeenea kwenye sekta ya mafuta ya Liberia hata kabla ya mafuta kugunduliwa .
Global Witness ilisema jana kuwa maafisa wa serikali na kampuni moja zimetoa rushwa kupata kandarasi . Ripoti hiyo pia imeishutumu serikali kwa kuwapa mikataba ya mafuta kampuni zisizo na uzoefu kabisa au uzoefu mdogo wa kazi hiyo.
Mpiga kampeni mkuu wa Global Witness Natalie Ashworth amesema serikali imefanya baadhi ya mabadiliko ya kutia moyo kuweza kuongeza uwazi na mabadiliko katika makampuni ya mafuta lakini anasema mabadiliko haya yamefanyika kwa udhaifu mkubwa , na kusema baadhi ya maafisa wa serikali wameamua kuvunja sheria zao wenyewe.