Ufaransa yatangaza itafungua sehemu za kumbukumbu zake za kitaifa za vita vya uhuru wa Algeria

Bendera za Ufaransa na Algeria zikipepea kwenye moja ya majengo ya kumbukumbu

Kati ya mwaka 1954 na 1962 Ufaransa ilifanya vita dhidi ya vuguvugu la kudai uhuru katika koloni lake la wakati huo. Maelfu ya wa Algeria waliuawa na majeshi ya Ufaransa pamoja na washirika wao walitumia  mateso dhidi ya wapinzani kulingana na wana historia

Ufaransa ilitangaza Ijumaa kuwa hivi karibuni itafungua kwa umma sehemu zilizoainishwa za kumbukumbu zake za kitaifa kuhusu vita vya uhuru wa Algeria na kutoa mwangaza kutokana na baadhi ya mtazamo mbaya zaidi katika historia ya karne ya 20 ya Ufaransa.

Kati ya mwaka 1954 na 1962 Ufaransa ilifanya vita dhidi ya vuguvugu la kudai uhuru katika koloni lake la wakati huo. Maelfu ya wa Algeria waliuawa na majeshi ya Ufaransa pamoja na washirika wao walitumia mateso dhidi ya wapinzani kulingana na wana historia.

"Tunahitaji kuwa na ujasiri wa kuangalia ukweli wa kihistoria unaotukabili, waziri wa utamaduni wa Ufaransa, Roselyne Bachelot alisema wakati alipotoa tangazo kuhusu kufungua kumbukumbu hiyo".

Maandamano huko Paris Julai 5,2020 kuunga mkono vuguvugu la Hirak la Algeria ilipoadhimisha kumbukumbu ya uhuru wake 1962

Mapigano ya Algeria yaliivuruga Ufaransa na kuchochea jaribio la mapinduzi lililoshindwa dhidi ya Rais wa wakati huo Charles de Gaulle ili kumzuia kukomesha utawala wa Ufaransa. Takribani miaka 60 baada ya kumalizika mzozo, lakini mzozo huo bado ni mada nyeti na inayoleta mgawanyiko nchini Ufaransa.

Kuondoa uainishaji wa kumbukumbu ni hatua muhimu kuelekea uelewa mzuri wa vita, kulingana na Benjamin Stora, mwanahistoria mkuu wa kifaransa wa Algeria.