Ufaransa yakabidhi kambi ya kijeshi Chad

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron

Ufaransa imekabidhi kambi yake ya kwanza ya kijeshi kama sehemu ya kujiondoa kijeshi kutoka Chad, majeshi ya Ufaransa na Chad yamesema Alhamisi.

Mkuu wa kijeshi wa maswala ya itifaki wa Chad amesema kambi iliyoko kaskazini mwa nchi imekabidhiwa na kwamba itatoa taarifa kwa umma kuhusu maendeleo ya kuondoa vikosi vya ufaransa katika kambi kwenye mji wa mashariki wa Abeche na mji mkuu Njamena.

Makabidhiano hayo yamefanyika kwa kufuata kalenda na masharti yaliyokubaliwa na Chad, mkuu wa jeshi wa maswala ya itifaki alisema katika wakati tofauti.

Mwezi uliopita Chad ilisitisha ghafla operesheni za kijeshi na mtawala wake wa zamani na vikosi vya ufaransa vilianza kuondoka kwenye nchi ijumaa iliyopita siku kumi baada ya ndege za kivita kuondoka.

Hatua hiyo inakuja wakati ambapo Chad inafanya uchaguzi wa bunge na serikali za mitaa jumapili.