Ufaransa kurudisha kazi za Sanaa za Afrika

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, alkipiga picha na watu na baadhi ya watu kwenye mkutano wa Ufaransa na bara la Afrika 2021 huko Montpellier, kusini mwa Ufaransa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anasema nchi yake itarudisha kazi za sanaa 26 za Kiafrika nchini Benin baadaye mwezi huu

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anasema nchi yake itarudisha kazi za sanaa 26 za Kiafrika nchini Benin baadaye mwezi huu. Majadiliano yamekuwa yakiendelea kwa miaka kadhaa juu ya kurudisha kazi za sanaa kutoka kwa Ufalme wa Dahomey wa karne ya 19.

Inayoitwa "Hazina ya Abomey," viti vya enzi vya kifalme, madhabahu ya sherehe, sanamu zilizoheshimiwa na vipande vingine kwa sasa vimekaa katika Jumba la kumbukumbu la Quai huko Paris. Macron alisema katika mkutano wa Afrika na Ufaransa huko Montpellier Ijumaa kazi za sanaa za Benin zitarejeshwa mwishoni mwa Oktoba, kwa sababu kurudisha kazi hizi kwa Afrika ni kuwapa vijana wa Kiafrika uwezo wa kuona tamaduni zao."

Kitendo hicho ni sehemu ya mipango ya Ufaransa iliyoahidiwa kwa muda mrefu ya kurudisha sanaa iliyochukuliwa kutoka Afrika wakati wa ukoloni.