Uchunguzi juu ya chanzo cha ajali ya Egypt Air waendelea

Ndege ya shirika la ndege la Egypt Air

Timu ya uchunguzi katika bahari ya Mediterranean inaangalia mabaki ya ndege ya shirika la ndege la Egypt Air inayoaminika kupata ajali kwenye anga ya bahari wakati ikisafiri kuelekea Cairo, Misri ikitokea Paris nchini Ufaransa.

Ripoti za awali kwamba mabaki ya ndege hiyo yalionekana karibu na kisiwa cha Greek hazikuwa sahihi. Maafisa hivi sasa wanasema kwamba hawajathibitisha kupata mabaki yeyote kutoka kwenye ndege hiyo.

Misri inasema ugaidi huwenda ikawa chanzo kikuu cha janga hilo kuliko matatizo ya kiufundi lakini hakuna taarifa kamili inayoelezea juu ya chanzo cha janga hilo. Ndege hiyo aina ya Airbus ikiwa na abiria 66 iligeuza haraka na kupoteza mara moja mwelekeo kabla ya kudondoka na kupotea kutoka kwenye rada mapema Alhamis.