Zaidi ya wiki moja baada ya uchaguzi wa duru ya pili kwenye visiwa vya Comoro matokeo bado yamegubikwa na utata.
Makamu Rais wa Comoro, Mohamed Ali Solihi, amepinga matokeo yaliyompa ushindi kiongozi wa zamani wa mapinduzi Azali Asoumani. Mgombea aliyeshika nafasi ya tatu Gavana Mouigni Baraka wa Grande Comore pia amepiga matokeo hayo.
Makamu Rais Solihi ametoa wito wa kurudiwa uchaguzi katika kisiwa cha Anjouan, moja ya visiwa vitatu, kwa sababu anasema matokeo kutoka vituo 23 kati ya 400 vilitarajiwa kumuunga mkono.
Mohamed Mshangama, rais wa taasisi ya matumizi ya jamii wa Comoro, amesema hali bado ni ya wasi wasi huko Comoro huku makamu Rais Solihi akiomba mahakama ya katiba kutoa uamuzi juu ya uhalali wa matokeo katika kisiwa cha Anzouan.