Uchaguzi wa urais wa marudio sasa utafanyika tarehe 26 mwezi Oktoba. Kupitia taarifa siku ya Alhamisi, tume ya uchaguzi na mipaka IEBC ilisema kuwa tarehe hiyo imebadilishwa ili kuwapa wadau muda wa kutosha kujitayarisha kwa zoezi hilo.
Uchaguzi huo ulikuwa umepangwa kufanyika tarehe 17 baada ya mahakama ya juu kubatilisha matokeo yaliyokuwa yametangazwa na tume hiyo, kwamba rais Uhuru Kenyatta alikuwa ameshinda.
Uchaguzi mkuu ulifanyika tarehe nane mwezi Agosti na baadaye mgombea wa urais kwa tikiti ya muungano wa NASA, Raila Odinga, akawasilisha hoja mahakamani kutaka uchaguzi huo ubatilishwe na kudai kwamba uligubikwa na dosari.