Hali ya mvutano umeshuhudiwa nchini humo tangu kumalizika kwa muhula wa rais aliyeko madarakani mwaka jana bila kufanyika kwa zoezi hilo. mamlaka ya uchaguzi imeorodhesha wagombea 39 wakiwemo rais wa sasa Mohamed Abdullahi Mohamed, wengine wawili waliowahi kuwa marais, mmoja aliyewahi kuwa waziri mkuu, maafisa wa ngazi za juu pamoja na mwanahabari mmoja miongoni mwa wengine.
Vile vile kuna mwanamke mmoja kwa jina Fawzia Yusuf Haji Adam ,ambaye ni mbunge aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya kigeni nchini humo.Uchaguzi huo unafanyika wakati usalama ukiwa umedorora kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kundi la kigaidi la al Shabab linalopinga serikali , kwenye mji mkuu pamoja na maeneo mengine nchini. Shambulizi la kujitoa muhanga la Jumatano liliua takriban watu wanne wakiwemo wanajeshi wawili wa serikali kwenye kituo kimoja cha ukaguzi karibu na uwanja wa ndege wenye ulinzi mkali, ambapo wabunge watakutana Jumapili, ili kuchagua rais mpya.