Waziri wa zamani Liberia, Ngafuan, atangaza kuwania Urais

Augustine Ngafuan, Minister of Foreign Affairs of Liberia, speaks to the media.

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Liberia, Augustine Ngafuan, ametangaza rasmi kuingia katika mbio za kuwania urais katika taifa la Afrika Magharibi la Liberia katika uchaguzi wa mwakani.

Katika orodha ya wagombea kuna Makamu wa Rais wa sasa, Joseph Boakai, mwanasoka na mchezaji bora wa dunia wa zamani, George Weah wa chama cha Congress for Democratic Change, Charles Brumskine wa chama cha Liberty, mfanyabiashara Benoni Urey, na mshirika wa rais wa zamani Charles Tylor.

Bwana Ngafuan ambaye alihudumu kama waziri wa fedha katika utawala wa rais Ellen Johnson Sirleaf ameiambia VOA kwamba ana rekodi nzuri ya utendaji na uwajibikaji katika uongozi wa umma na sekta ya binafsi.