Uchaguzi katika kaunti nne za Kenya waahirishwa tena

Wafuasi wa upinzani wawasha moto kwenye barabara na kuandamana nchini Kenya wakipinga uchaguzi wa urais wa marudio. Oktoba 27, 2017.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na mipaka ya Kenya, IEBC, alitangaza Ijumaa jioni kwamba uchaguzi uliopangwa kufanyika katika kaunti nne siku ya Jumamosi umeahirishwa.

Wafula Chebukati alisema kuwa baada ya kushauriana na makamishna na maafisa wa tume hiyo, "tumeonelea ni jambo la busara kuahirisha uchaguzi huo uliopangwa kufanyika hapo kesho Jumamosi hadi tarehe ambayo tutaitangaza baadaye."

Uchaguzi katika kaunti za Migori, Kisumu, Siaya na Homa Bay ulikuwa umeahirishwa hadi Jumamosi kufuatia ghasia zilizozuka katika maeneo mbalimbali.

Chebukati alisema IEBC ilichukua hatua hiyo ya kuahirisha tena zoezi hilo kwa sababu za ya kiusalama.

Hata hivyo, mwenyekiti huyo alisema kuwa uchaguzi utaendelea katika vituo ambazo kaunti ya Turkana