Leban Seyoum ni mtu mwenye bidii sana. Anafanya kazi masaa mengi akiendesha kampuni ndogo ya usafiri yenye magari makubwa ya mizigo.
“Tutaiacha iendelee kuwaka kwa dakika chache," anasema.
Alikuja Marekani na familia yake alipokimbia vita kati ya Ethiopia na Eirtrea mwaka 2000.
Leban Seyoum, mfuasi wa Trump anaeleza:“Waliwalazimisha watu kuondoka katika nchi zao na hivyo kusababisha matatizo mengi kwa familia nyingi wakati huo, familia nyingi kwa kweli zilihamia hapa nchini.”
Seyoum anajiona kama ni mconservative katika masuala ya fedha na kijamii na ni mfuasi mkubwa wa rais wa zamani Donald Trump.
Anaeleza kuwa: “Wakati, Rais Trump alipokuwa madarakani, mambo yalikuwa mazuri, kibiashara. Unajua, soko lilikuwa zuri, fursa za kazi zilikuwa kubwa, na watu walikuwa na matumaini.”
Biashara ya usafirishaji ni kazi kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta na yeye anamlaumu Biden.
Seyoum, mfuasi wa Trump anasema: “Hivi sasa, bahati mbaya, huku bei za mafuta zikiwa juu, ziko katika kiwango cha dola 5 kwa dizeli, dola 5 na nusu kwa dizeli. Na hii inazifanya biashara nyingi kutopata faida. Kama mnavyofahamu, usafiri ni uti wa mgongo Marekani. Takriban asilimia 70 ya bidhaa zinasafirishwa na magari makubwa kama haya.”
Bei za mafuta ulimwenguni zimekuwa tete sana na kuchangiwa na mchanganyiko wa vigezo kadhaa. Leban anasisitiza kuwa Rais wa zamani Trump ana jibu.
Seyoum alisema: “Trump ametuonyesha jinsi ya kufanya shughuli hizi. Unachimba, unachimba, unachimba. Halafu, unashindana. Unaona, hivi sasa, hatuhitaji kuangazia itikadi nyingine.”
Wademocrat, kama Fatmata Barrie, anaona uamuzi katika uchaguzi huu uko tofauti sana. Alikuja nchini Marekani akiwa katika umri wa miaka 11 kutoka kwenye nchi yake ya asili Sierra Leone. Baada ya kusomea sheria alihamia Maryland ili kufanya kazi ya utetezi na sheria za uhamiaji.
Fatmata Barrie, mfuasi wa Kamala Harris anasema: “Ndoto yangu ilikuwa ni aina fulani ya kazi ambapo naweza kufanya kazi katika jamii nab ado kuwa na maisha mazuri na kuishi vizuri.”
Fatmata ni mtetezi mkubwa wa haki za kiraia, haki za wanwake, na wahamiaji. Yeye anamuunga mkono Kamala Harris katika uchaguzi wa Novemba mwaka huu.
Barrie anaongeza kuwa:
“Nadhani Makamu Rais Kamala Harris ni mtu wa watu. Yeye ni mtu ambaye tunamhitaji hivi sasa kuondoa mugawanyiko uliopo katika nchi hii.”
Ana wasi wasi kuhusu Trump kushinda tena urais.
Anasema kuwa:“Nina khofu. Khofu ya kuwa wahamiaji ndiyo kwanza wanaanza tena maisha. Khofu ya kuwa watu weusi na wengine wasio wazungu wanaanza tena. Ni vigumu wakati mtu aliye juu anaongoza halafu kila mtu hajihisi vizuri.”
Anasema kama yaliyopita yanatoa muongozo wowote, wahamiaji wanafuatilia mchakato wa kisheria ambao utakuwa ambao utaingiliwa na mpango wa Trump wa kuwafukuza kutoka nchini Marekani mamilioni ya wahamiaji wasiokuwa na nyaraka.
Fatmata alieleza:
“Wanapokwenda kuhojiwa, wanafanya kihalali, wanatiwa ndani, na kushikiliwa huko. Baadhi wamefukuzwa nchini wakati hawakutakiwa kufukuzwa.”
Leo, anafanya kazi ya kujitolea kwenye benki ya chakula.
Anasema ingawaje viashiria vya uchumi vina nguvu wengi bado wanapambana.
Fatmata anasema:“Namba zinaonekana ziko vizuri. Lakini kuna watu hawapo ambao siyo siku zote tunawafikiria kama watu wanaolipwa ujira kwa saa, watu walioko huko wana familia ya watu wawili au watatu wanaishi katika nyumba moja.”
Anaeleza kuwa:“Kimsingi tofauti iko juu, ni asilimia 0.1 watakuwa na fedha na wengine kama sisi tutakuwa tunapambana kama mtaamua kumchukua Trump. Taifa halijajengwa hivyo. Marekani imekuwa Marekai kwasababu ya kazi za daraja la wafanyakazi walivyofanya katika nchi hii, ndiyo walioijenga Marekani.”
Mitizamo miwili ya dhahiri kwa Marekani, maamuzi mawili muhimu kwa siku zijazo.
Imetayarishwa na mwandishi wetu Hubbah Abdi, VOA Washington