Jimbo la Georgia lafanya uchaguzi maalum Marekani

Jengo la Bunge la Marekani

Wapiga kura wa jimbo la kusini mwa Marekani, Georgia, wanachaguwa muwakilishi wao katika uchaguzi maalumu wa baraza la wawakilishi Jumanne.

Uchaguzi huo unafuatiliwa kwa karibu na unaonekana ni mtihani kwa chama cha Republican chini ya utawala wa rais Trump na mustakabal wa chama katika bunge hapo mwakani.

Umhimu uliowekwa na vyama vya Republikan na Demokrat ni ushahidi kwamba fedha zimetumika vya kutosha na pande zote, inaelezwa ni zaidi ya dola milioni 50 ikiwa ni kiwango kikubwa kutumika kwa uchaguzi wa bunge.

Mgombea wa Demokrat ni mfanyakazi wa zamani wa bunge Jon Ossof mwenye umri wa miaka 30 akigombea kwa mara ya kwanza na ambaye alishinda katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo lakini hakupata kura za kutosha kwa mujibu wa kanuni.

Mgombea wa Republikan ni Karen Handel mwenye miaka 55 ambaye ni waziri wa zamani wa mambo ya nje wa jimbo la Georgia.