Ubelgiji itapima maji machafu kutoka kwenye ndege zinazowasili kutoka China kwa ajili ya aina mpya ya virusi vya COVID.
Hii ni kama sehemu ya hatua mpya za kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona huku maambukizo nchini China yakiongezeka, serikali ilitangaza Jumatatu.
Hii itakuwa ni juhudi za ziada za ufuatiliaji ili kuhakikisha kwamba taarifa tunazopokea kutoka China ni sahihi, alisema Steven Van Gucht wa taasisi ya kitaifa ya afya ya umma wakati akiongea na Reuters.
Alisema Ubelgiji inafahamu kuwa baadhi ya abiria walioambukizwa COVID wanaweza wasitumie choo wakati wa safari zao za ndege, na kwa hivyo hatua hiyo mpya haikusudii kufuatilia watu lakini ni kufuatilia kwa uhuru kile kinachotokea China.
Ubelgiji pia inawataka wasafiri kutoka China kupimwa COVID-19 ikiwa wanaonyesha dalili siku saba baada ya kuwasili.