Umoja wa Falme za Kiarabu Jumatano umekubali utambulisho cha balozi wa Taliban katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta katika Ghuba ya Kiarabu, ikiwa ni mapinduzi makubwa ya kidiplomasia kwa watawala wa Afghanistan, ambao hawatambuliwi rasmi kama serikali halali ya nchi hiyo.
Maendeleo hayo, ambayo yanamleta balozi wa kwanza wa Taliban toka alipoteuliwa wa China Desemba mwaka jana, yanaleta mgawanyiko wa kimataifa kuhusu jinsi ya kafanyakazi na serikali ya sasa ya Kabul.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Kabul ilithibitisha habari hiyo ya uteuzi wa Badruddin Haqqani, katika taarifa ya mtandao wa X.
Wizara hiyo haikujibu maombi ya majibu kuhusu Haqqani, ambaye hapo awali alikuwa mjumbe wa Taliban nchini UAE.