Tuzo ya amani ya Nobel yapewa mwanaharakati wa Belarus, na makundi mawili ya haki za binadamu ya Russia na Ukraine

Mkuu wa kamati ya Nobel Berit Reiss Andersen, akitangaza washindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka wa 2022, mjini Oslo, Oktoba 7, 2022.

Tuzo ya amani ya Nobel mwaka huu imepewa Ales Bialiatski, mwanzilishi wa vuguvugu la kutetea demokrasia katikati ya miaka ya 80 nchini Belarus , pamoja na makundi mawili ya kutetea haki za binadamu, Memorial ambalo ni shirika la Russia na kituo cha kutetea uhuru wa raia cha huko Ukraine.

Tuzo ya amani ya Nobel ya mwaka uliopita ilipewa Maria Ressa kutoka Ufilipino na Dmitry Muratov, raia wa Russia. Kamati ya Nobel Ilisema wawili hao walitunukiwa” kwa sababu ya juhudi zao za kulinda uhuru wa kujieleza, ambao ni sharti la kufikia demokrasia na amani ya kudumu.”

Tuzo ya Nobel ya karibu dola milioni 1 hutolewa pia pamoja na medali ya dhahabu

Muratov aliuza medali yake ya Nobel ili kusaidia watoto wa Ukraine waliohamishwa kwenye makazi yao na vita. Tajiri mfadhili ambaye hakutaka jina lake litajwe alinunua medali hiyo ya dhahabu dola milioni 103.5.