Uturuki yaomba Russia msamaha kwa kuuwawa kwa rubani wake

Robot Test JPG METADATA nasa 201512150014.jpg 2018-11-21 11:21:16

Robot Test JPG METADATA nasa 201512150014.jpg 2018-11-21 11:21:16

Rais wa Uturuki amewasiliana na rais mwenzake wa Russia akielezea sikitiko la kuangushwa kwa ndege ya kijeshi ya Russia na mwanajeshi wa kituruki hapo November. Matumaini kuwa uhusiano baina ya pande hizo mbili utaboreka, lakini shutuma dhidi yao zitaendelea.

Barua inayoelezea rambi rambi kutoka kwa rais Recep Tayyip Erdogan kwa rais wa Russia Vladamir Putin, imetumwa wakati serikali ya Uturuki inapoanza tena uchunguzi dhidi ya mwanamume raia wa uturuki anayelaumiwa na Moscow kwa kupiga risasi na kumuuwa rubani aliyekuwa anaruka kwa kutumia parachute kutoka kwenye ndege yake iliyokuwa inaanguka.

Hadi sasa Erdogan ametetea kwa dhati kuangushwa kwa ndege hiyo ya Russia, ambayo Ankara inailaumu kwa kukiuka anga ya uturuki ilipokuwa ikiruka kutoka kambi ya Syria.

Mwandishi wa masuala ya kidiplomasia kutoka gazeti la Uturuki la Cumhuriye na mtandao wa Al Monitor, Semih Idiz, anasema rais wa Ututurkki anakabiliana na vikwazo vya kisiasa na kiuchumi vilowekwa na Russia kwa Uturuki kufwatia kuangushwa kwa ndege hiyo ya Russia.

Vikwazo vinajumlisha kizuizi cha kusafirisha nje mazao ya chakula cha uturuki na watalii wa warussia wanaotaka kuzuru Uturuki.

Waziri mkuu wa uturuki Binali Yildirim alisema kuwa Erdowan atazungumza na rais Putin baadae wiki hii, katika kile kilichoripotiwa kuwa mazungumzo ya moja kwa moja baina ya viongozi hao wawili tangu November ilipoangusha ndege hiyo.

Ankara pia inashutumu Moscow kwa kulihami kundi la Kikurdi la waasi PKK na makombora , dai ambalo Russia inakana.

Moscow inadai msamaha kutoka kwa Ankara na fidia kwa familiya ya rubani wa Russia alouwawa.

Katika ishara kwamba Moscow inapokea hatua za uturuki , Russia imemualika waziri wa mambo ya nje wa uturuki kwa mkutano wa kikanda ijumaa.

Erdogan na serikali yake inaonekana kuwa na hamu ya kumaliza kile kinachonekana kuwa kutengwa kwa uturuki katika kanda. Serikali za Uturuki na Israel zilirudisha uhusiano wao wa kibalozi hapo Jumanne.