Tunisia imezindua mpango wa kuwasilisha maombi kuwania urais katika uchaguzi ujao wa Oktoba 6, huku kukiwa na kile ambacho wataalam wanasema ni vikwazo vikubwa kwa watu wenye matumaini ya kumpinga Rais aliyeko madarakani Kais Saied.
Masharti kadhaa na mahitaji ya kuwania wadhifa huo yamebadilika chini ya Saied, mwenye unmri wa miaka 66, ambaye alichaguliwa kidemokrasia mwaka 2019 lakini alifanya unyakuzi mkubwa wa mamlaka mwaka 2021.
Ili kustahiki kuwepo kwenye karatasi ya kura, wagombea wanatakiwa kukusanya idadi kubwa ya saini, alisema Amine Kharrat, mchambuzi wa siasa katika kituo huru cha uchunguzi cha Al Bawsala.