Hayo aliyasema wakati akifanya mazungumzo na Kansela wa Austria Kari Nehammer, ikielezewa kuwa ziara ya kwanza ya waziri mkuu wa India nchini humo baada ya miaka 41.
Kabla ya kutembelea Austria, Modi alitembelea Russia, hatua iliolalamikiwa vikali na Ukraine. Nehammer alisema ilikuwa muhimu kwa Austria kuelewa msimamo wa India kuhusu Ukraine, na kwamba ilikuwa “ muhimu na hatua kubwa” kwamba India ilishiriki kwenye kikao cha amani cha hivi karibuni nchini Switzerland.
Nehammer ameongeza kusema kuwa Austria itashikilia nafasi muhimu kama mpatanishi kuelekea amani ya Ukraine. Wakati akizungmza mbele ya wanahabari mjini Vienna, Modi alisema kua, “huu siyo wakati wa vita. Mambo hayawezi kutatuliwa kwenye uwanja wa mapigano.”
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy awali alilalamikia picha ya Modi akimkumbatia Putin, akisema kuwa ilikuwa pigo kubwa kwa juhudi za amani.Ziara ya Modi ya Russia ambako India ina uhusiano wa muda mrefu, ilkuwa ya kwanza tangu Russia ilipofanya uvamizi wa Ukraine.