Tume ya uchaguzi Chad yasema Mahamat Idriss Deby alishinda uchaguzi wa rais

Rais wa Chad Idriss Deby akiwasalimia wafuasi wake wa Patriotic Salvation Movement wakati wa mkutano katika mji mkuu N'djamena

Tume ya uchaguzi huko Chad lilisema Alhamisi kuwa Rais wa mpito Mahamat Idriss Deby alishinda uchaguzi wa urais wa Mei 6 kwa zaidi ya asilimia  61 ya kura, likitaja matokeo ya muda, wakati pia mpinzani wake mkuu alijitangaza kuwa mshindi.

Utawala wa kijeshi wa Chad umekuwa wa kwanza kati ya nchi zilizokumbwa na mapinduzi katika Afrika Magharibi na Kati kurejesha sheria ya kikatiba kupitia sanduku la kura, lakini baadhi ya vyama vya upinzani vimelalamika kilio chao kuhusiana na wizi wa kura.

Huku hali ya wasiwasi ikizidi, idadi kubwa ya vikosi vya usalama vimetumwa kwenye makutano makubwa katika mji mkuu N'Djamena kabla ya kutangazwa kwa matokeo.

Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Kusimamia Uchaguzi Ahmed Barticet alisema Deby amepata aslimia 61.3 ya kura bila shida ikiwa ni zaidi ya asilimia 50 inayohitajika ili kuzuia duru ya pili.