Tshala Muana akamatwa DRC

Mwanamziki wa DRC Tshala Muana (katikati)

Shirika la kutete haki za kibinadamu nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ACAJ, linataka maafisa wa usalama nchini humo kumwachilia huru mwanamziki maarufu Tshala Muana ambaye alikamatwa jumatatu mjini Kinshasa.

Polisi wamemkamata mwanamziku huyo mweye umri wa miaka 62 baada ya kutoa wimbo ambao wachambuzi nchini humo wanasema kwamba tafsiri yake inamdalilisha rais wa sasa Felix Tshisekedi, japo wimbo huo hautaji mtu yeyote.

Ujumbe katika wimbo huo kwa jina 'Ingratitude' unamlenga mtu ambaye amepewa kila analotaka maishani lakini amekosa kufanya mema wakati yupo madarakani.

Mwanamziki huyo ana uhusiano wa karibu san ana familia ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Joseph Kabila.

Kulingana na mwandishi wetu wa DRC Austere Malivika, Tshala Muana anazuiliwa na polisi ili kutoa maelezo zaidi kuhusu wimbo wake.

Wimbo huo umetolewa wakati kuna mvutano kati ya rais Tshisekedi na viongozi wa vyama vinavyomuunga vinavyoongozwa na watu walio karibu sana na rais mstaafu Joseph Kabila.

Maandamano yameripotiwa mjini Kinshasa baada ya kuripotiwa kwamba Tshala Muana amekamatwa.

Imetayarishwa na Kennes Bwire,VOA, Washington DC