Rais wa Marekani Donald Trump ameonyesha nia ya kutoa ushahidi mbele ya mwendesha mashitaka maalum anayechunguza kuingilia kati kwa Rashia katika uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 2016 na mambo mengine.
Maelezo ya rais yamekuja baada ya mmoja wa mawakili wake kuthibitisha anajitoa.
Trump alijibu angependa kufanya hivyo alipohojiwa na waandishi wa habari kutaka kujua kama ana nia ya kuhojiwa na wachunguzi.
Rais alitoa jibu hilo wakati akiondoka katika chumba cha kidiplomasia cha White house mara tu baada ya kusaini nyaraka ya kuelekeza utawala wake kuchukua hatua za kibiashara dhidi ya China.
Majibu ya Trump yalikuja baada ya taarifa kwamba mmoja wa mawakili wake John Dowd kuthibitisha kwamba anajitoa.