Trump akiri kupata taabu ya uungaji mkono kwenye chama chake.

Mgombea mtarajiwa wa chama cha republikan Donald Trump akizungumza na wafuasi wake, Feb. 26, 2016.

Mgombea mtarajiwa wa chama cha Republikan Donald Trump ameeleza kwamba anapata taabu kupata uungaji mkono wa maafisa wa chama cha Republikan , lakini jana jumanne alieleza wasi wasi kidogo kwamba yuko nyuma sana kwenye uchangishaji fedha dhidi ya mdemokrat Hillary Clinton kwa uchaguzi wa Novemba 8.

“Tuna chama ambacho ninamaanisha kwamba ninapata shida zaidi na watu waliomo humo kuliko ninavyopata taabu na wademokrat. Kwasababu hawataki kuniunga mkono Trump aliambia NBC.”Baadaye wataniunga mkono .Kwa kweli kama wasiponiunga mkono pia ni sawa.Nitashinda tu kwa njia yeyote.”

Bilionea huyo wa biashara za nyumba ambaye pia wakati fulani alikuwa mtangazaji wa kipindi cha TV cha maisha halisi -reality show alitathmini kampeni yake saa chache baada ya ripoti mpya kutoka ikieleza kuwa mpaka sasa kampeni hiyo imechangisha dola milioni 1.3 tu katika mwezi Juni ikilinganishwa na Hillary Clinton mwenye dola milioni 42.5.