Wakati akiwakaribisha Jumapili jioni, Trump alisema kuwa “ Nafikiri kuwa hilo litakuwa kwanza kwenye orodha yetu ya mazungumzo kwa kuwa lazima tumalize kuyashughulikia mambo yanayojiri hivi sasa hapa nchini.
Wachambuzi nchini Marekani wanasema kuwa majimbo tofauti hapa Marekani yana sheria mseto kuhusiana na umiliki wa bunduki na kwa hivyo kuna haja ya kuwepo mbinu tofauti za kukabiliana na tatizo hilo.
Pia kuna baadhi ya wanasiasa ambao wanafikiria kuwa huenda serikali kuu ikachukua hatua zake wakati wajumbe wa Congress pamoja na Senate wakirejea katika shughuli zao baada ya kuwa kwenye likizo ya wiki moja kwenye maeneo yao ya uwakilishi.
Mjadala nchini Marekani juu ya njia bora ya kukabiliana na mauaji mashuleni unaongeza kasi, lakini haijulikani iwapo mauaji hayo yatalifanya Bunge- Congress kuchukua hatua bado ni kitendawili.
Katika nchi ambayo Katiba ya Marekani inaruhusu umiliki wa silaha, wabunge hawakotayari kuweka sheria za udhibiti wa silaha, pamoja na kuwepo matokeo ya mauaji ya kutumia silaha miaka ya karibuni.
Mjadala kuhusu sheria za umiliki wa bunduki umekuwa ukiendelea baada ya mauji kwenye shule hilo lakini haijabainika iwapo Congress itachukua hatua.