Trump kukabiliana na China kwenye teknolojia ya AI

  • VOA News

Picha ya kisayansi ikonyesha mtambo wa AI kwenye kompyuta.

Hata kabla ya kuwepo ofisini kwa saa 48, rais wa Marekani Donald Trump alituma ujumbe wa kukabiliana na China kwenye anga za juu, na kwamba utawala wake utakuwa na ajenda kubwa ifikapo kuendesha Marekani mbele  kwenye teknolojia ya akili mnemba au AI pamoja na miundombimu inayoiendesha.

Kwenye siku yake ya kwanza ofisini, alibatilisha amri ya kiutendaji iliyotiwa saini 2023 na rais Joe Biden ikilenga kudhibiti mwendelezo wa AI yenye nguvu zaidi, na badala yake kuweka mikakati ya kuhakikisha ubinafsi unalindwa, haki za kijamii pamoja na usalama wa kitaifa.

Siku iliyofuata Trump alikutana na viongozi wa makampuni makubwa ya teknolojia akiwemo Sam Altman, Mkurugenzi mkuu wa Open AI, Larry Ellison, mwenyekiti wa Oracle na Masayoshi Son, Mkurugenzi mkuu wa SoftBank, na kutangaza uwekezaji wa dola bilioni 500 kwenye mfumo wa AI unaojulikana pia kama Stargate.

Stargate inalenga kuwekeza katika kubuni hadi vituo 10 vikubwa vya data hapa Marekani ambavyo vitatoa huduma za kompyuta kwa mifumo ya AI. Kituo cha kwanza tayari kinajengwa Texas. Uwekezaji huo unatarajiwa kuunda hadi ajira 100,000 wakuu wa makampuni hayo wamesema.