Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, amepangiwa kuhojiwa na maafisa wa uangalizi wa New York, leo hii, hatua inayohitajika kabla ya hukumu yake ya Julai katika kesi yake ya uhalifu ya kulipa fedha za “kumnyamazisha mtu” kwa mujibu wa watu watatu wanaofahamu mpango huo.
Trump atafanya atahojiwa kupitia mkutano wa njia ya video kutoka katika makazi yake ya Mar-a-Lago, ya Palm Beach, Florida, watu hao wameiambia shirika la habari la The Associated Press.
Walizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao kwa sababu hawaja idhinishwa kuzungumzia mipango hiyo hadharani.
Mmoja wa mawakili wa Trump, Todd Blanche, atakuwepo kwenye mahojiano hayo. Watu waliotiwa hatiani ya uhalifu New York kwa kawaida hukutana na maafisa wa uangalizi bila mawakili wao, lakini jaji katika kesi ya Trump, Juan Merchan, amesema kwa njia ya barua Ijumaa kwamba angeruhusu uwepo wa wakili wa Trump Blanche.