Baraza hilo lenye wajumbe tisa, wanaume sita na wanawake watatu, lilifikia uamuzi wake baada ya saa tatu yz mashauriano, mara ya kwanza Trump kumtaka awajibishwe kwa madai yaliyoenezwa kwa miaka mingi kutoka kwa wanawake waliomtuhumu kutaka kutenda nao ngono bila ridhaa yao.
Baraza hilo la mahakama lilitupilia mbali madai ya E.Jean Carrol, ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 79, kwamba Trump alimbaka katika chumba cha kubadilishia nguo katika duka la Bergdorf Goodman mjini New York wakati fulani mwaka wa 1996.
Lakini liliamua kuwa alimnyanyasa kingono, na kuomba alipwe fidia ya dola milioni 2 kwa madai hayo.
Liliomba Caroll alipwe fidia nyingine ya dola milioni 3 kutokana na madai yaliyotolewa mara kwa mara hadharani na Trump kwenye mitandao yake ya kijamii kuwa madai ya Caroll yalikuwa ulaghai na utapeli mtupu.