Trump arejea Washington

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alipokuwa akizungumza na wafuasi wake.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump anarejea mjini Washington kwa mara ya kwanza tangu kuondoka madarakani. Atatoa hotuba ya sera Jumanne usiku mbele ya washirika ambao wamekuwa wakitayarisha ajenda ya uwezekano wa muhula wa pili.

Trump atahutubia Mkutano wa Siku mbili wa First Policy Institute ya Marekani . Baadhi ya washauri wanamtaka atumie muda mwingi kuzungumzia maono yake ya siku zijazo na muda mchache wa kuzungumzia uchaguzi wa 2020 anapojitayarisha kutangaza kampeni inayotarajiwa ya Ikulu kwa mwaka 2024.

Wapinzani wake watarajiwa wa mwaka 2024, ni pamoja na Makamu wa Rais wa zamani, Mike Pence, wamekuwa wakichukua hatua za wazi zaidi kupinga hadhi ya Trump kama mpeperushaji bendera ya chama cha Republikan.