Trump apigwa tena faini kwa maoni yake nje ya mahakama

Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trumo, aliitwa kwenye kizimba cha utetezi kutoa ushahidi, na kupigwa faini ya dola 10,000 baada ya jaji kuhitimisha kwamba alikiuka kanuni za mahakama katika kesi yake ya kughushi.

Hii ni mara ya pili katika kipindi cha chini ya wiki mbili kwa Trump kupigwa faini kwa matamshi yake anayotoa nje ya mahakama licha ya jaji kumpiga marufuku kufanya hivyo.

Kabla ya kutoa faini ya sasa, Jaji Arthur Engoron alimwita Trump kwenye kizimba cha utetezi kutoa ushuhuda wa maneno yake kwa wanahabari saa kadhaa mapema kuhusu mtu ambaye ana mrengo mkubwa wa kisiasa ambaye yupo na jaji.

Trump na wakili wake wamesema kwamba maoni yake yalikuwa yakimuhusu aliyetoa ushuhuda Michael Cohen, ambaye ni mwanasheria wa zamani wa Trump, na si mhudumu wa mahakama.

Alimwambia jaji kutoka kizimba cha utetezi kwamba matamshi yake kuhusu mrengo wa kisiasa ulikuwa ukimlenga jaji mwenyewe na Michael Cohen.