“Nafikiri wakati umewadia,” Trump amesema katika mkutano wa kisiasa katika eneo la kuegesha ndege huko mji wa Moon, Jimbo la Pennsylvania.
Kim ni “mtu aliyesambaza silaha za nyuklia kila mahali,” lakini hivi sasa “hatorusha tena makombora hewani” wakati mpango uko njiani wa mkutano wa ana kwa ana ambao ni wakipekee kati ya kiongozi wa Korea Kaskazini na Marekani, Trump amesema.
Ameongeza kuwa wakati atakapokutana na Kim, “ Inawezekana nikaacha mkutano kwa haraka au tunaweza kukaa pamoja naye na kufikia makubaliano ya kipekee kwa manufaa ya dunia.”
Trump amedai kuwa ni juhudi zake zilizowezesha michezo ya Olympic ya kipindi cha baridi kufanikiwa ambayo iliandaliwa na Korea Kusini hivi karibuni, akiongeza kuwa bila ya juhudi zake za kudhibiti tishio la shambulizi la nyuklia, michezo hiyo “isingefanikiwa kabisa.”