Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, Jumatano aliiomba Mahakama ya Juu ya Marekani kubatilisha uamuzi wa kuzuia ugombea wake katika jimbo la Colorado, na kuanzisha mzozo wa hali ya juu kuhusu iwapo kifungu cha katiba kinachokataza wale wanaojihusisha na uasi kitamaliza medani zake za kisiasa.
Trump alikata rufaa dhidi ya uamuzi ulioungwa mkono na majaji 4 dhidi ya 3 mwezi Desemba na Mahakama ya Juu ya Colorado ambayo ilikuwa mara ya kwanza katika historia kutumia kifungu cha 3 cha marekebisho ya 14 ya katiba ambacho kilitumiwa kumzuia mgombea urais kuwepo kwenye karatasi ya kura.
Mahakama iliona kwamba ushiriki wa Trump katika tukio la Januari 6, 2021, katika bunge la Marekani lilimnyima haki chini ya kifungu hicho.
Sheria hiyo imetumika kwa kiasi kidogo katika historia ya Marekani, na hivyo Mahakama ya Juu ya Marekani haina uamuzi wa mfano juu ya shauri hilo.