Trump aahidi kurudisha nidhamu Marekani

  • Abdushakur Aboud

Donald Trump akila kiapu kwa ajili ya mhula wake wa pili White House.

Akizungumza baada ya kula kiapo kama rais wa 47 wa Marekani siku ya Jumatatu Januari 20, 2025, ndani ya ukumbi wa Rutanda katika jengo la bunge, Rais Trump amesema ataleta mapinduzi katika maisha ya Wamarekani.

Trump aliyenusurika kutokana na mashataka ya kuondolewa madarakani, mshtaka kadhaa ya uhalifu na majaribio mawili ya kutaka kuuliwa, alipata ushindi kwa muhula mwengine katika White House, amesema atachukua hatua muhimu za kiutendaji mara tu baada ya kuapishwa.

Akimaliza sherehe za kuapishwa bungeni kiongozi huyo ataelekea katika ukumbi wa Capital One Arena ambako karibu wafuasi wake elfu 20 wamekuwa wakifuatilia sherehe na kumsubiri kumkaribisha kama rais mpya wa Marekani.

Trump atia saini hati za kuchukua madaraka kwa awamu ya pili.

Hapo atatia saini amri karibu 100 za utendaji kuhusiana na mambo mbali mbali aliyoahidi atafanya siku ya kwanza baada ya kuchukua madaraka, miongoni mwao ni amri ya kutangaza hali ya dharura ya uhamiaji, hali ya dharura ya nishati na mambo mengine muhimu.

Akitangaza kwamba serikali inakabiliwa na "mzozo wa uaminifu," Trump amesema katika hotuba yake ya kwanza kwamba chini ya utawala wake "uhuru wetu utakombolewa tena. Usalama wetu utadumishwa. Wizani wa sheria utarekebishwa."