Tripoli yashambuliwa kwa mabomu

Maeneo yaliopigwa mabomu Tripoli.

Milipuko mikubwa ilifuatia mashambulizi mengine ya anga ya NATO jumatatu.

Milipuko mitano imesikika katika mji mkuu wa Libya Tripoli mapema Jumanne, ikiaminika kuwa ni mashambulizi ya ndege ya NATO.

Milipuko hiyo isiyo ya kawaida ilifuatia mashambulizi mengine ya anga ya NATO Jumatatu dhidi ya ghala za silaha za serikali karibu na mji wa magharibi wa Zintan.

Katika mji wa bandarini uliozingirwa wa Misrata wapiganaji waasi wamesema wamerudisha nyuma majeshi ya serikali kutoka vituo vinavyo zingira mji huo.

Wakati huo huo meli moja iliyokodishwa na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundi iliwasili Misrata Jumatatu imesafirisha vikopo 8,000 vya vyakula vya watoto pamoja na vifaa vinavyohitajika sana vya upasuaji na madawa.

Mapema Jumatatu Umoja wa Matiafa ulitangaza kwamba meli iliyokuwa inawasafirisha wakimbizi 600 kutoka Libya ilizama Ijumaa nje ya pwani ya nchi hiyo, na idadi ya walofariki haijulikani baado.